Waris Kareem kutoka Nigeria amekuwa gumzo kubwa katika mitandao ya kijamii kufuatia kipaji chake cha kuchora. Akiwa na zaidi ya wafuasi 100,000 kwenye Instagram, yeye ni miongoni mwa watoto waliojaaliwa talanta nchini Nigeria na anatumai kuitumia kusaidia nchi yake.