1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyeokolewa kutoka pangoni 2018 afariki Uingereza

16 Februari 2023

Mmoja wa wavulana 12 waliookolewa kutoka pango lililofurika nchini Thailand mwaka 2018 amefariki nchini Uingereza alikokuwa anasoma.

Screenshot aus einer DW-Produktion von Jack Parrock
Picha: DW

Kijana huyo Duangpetch Promthep, alipatikana akiwa amepoteza fahamu chumbani kwake katika Chuo cha Brooke House siku ya Jumapili.

Alipelekwa hospitalini, ambapo alifariki Jumanne. Sababu ya kifo chake haijabainishwa, lakini polisi wamesema haishughulikiwi kama suala la mashaka.

Soma pia:Zaidi ya 30 wauawa katika mashambulizi ya chekechea Thailand

Dom alikuwa nahodha wa Wild Boars, timu ya kandanda ya vijana katika mkoa wa kaskazini mwa Thailand wa Chiang Rai.

Wachezaji 12 wa timu hiyo na kocha wao walinaswa kwenye pango la Tham Luang Juni 2018.

Walipatikana siku tisa baadaye kwenye chumba kilichofurika, kilomita 4 kutoka kwenye mlango wa mapango, na zilipita siku nane nyingine kabla ya wote kuokolewa salaama.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW