1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mvutano kati ya Canada na India wazidi kuongezeka

15 Oktoba 2024

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, ameishtumu India kwa kufanya "kosa la kimsingi," huku mzozo ukiongezeka juu ya mauaji ya kiongozi wa jamii ya Singasinga inayotaka kujitenga Hardeep Singh Nijjar.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mjini Ottawa mnamo Oktoba 14, 2024
Waziri mkuu wa Canada Justin TrudeauPicha: Dave Chan/AFP

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Ottawa Trudeau alisema vitendo vya India ''havikubaliki''.

Soma pia:Canada yatangaza kusitisha ofisi za kibalozi India

Awali Trudeau alisema kuwa kulikuwa na "madai ya kuaminika" yanayohusisha huduma za kijasusi za India na mauaji ya Nijjarhayo.

India yasema madai ya Canada dhidi yake  ni ya kuiharibia sifa kwa manufaa ya kisiasa

Hapo jana India iliyataja madai hayo ya Canada kwamba ilihusika na mauaji ya mwanaharakati huyo wa Singasinga kama mbinu ya kuiharibia jina India kwa manufaa ya kisiasa.

Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, imesema kuwa Indiaina haki ya kuchukua hatua zaidi kujibu uungaji mkono wa serikali ya Trudeau kwa itikadi kali, vurugu na kujitenga dhidi ya India.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW