1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano kati ya Marekani na Iran wazidi makali

24 Aprili 2026

Mvutano kati ya Marekani na Iran kuhusu Mlango Bahari wa Hormuz umezidi makali leo Ijumaa.

Boti za jeshi la Iran
Rais Donald Trump wa Marekani ameamuru jeshi la nchi hiyo kuzishambulia boti ndogo za kijeshi za Iran kwenye Mlango Bahari wa Hormuz. Picha: IRIB TV/AFP

Hayo ni baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuamuru jeshi la nchi hiyo kuzishambulia boti ndogo za kijeshi za Iran kwenye ujia huo muhimu bahari kwa usafirishaji mafuta duniani.

Trump alitoa amri hiyo baada ya jeshi la Marekani kutangaza kuikamata meli nyingine ya mafuta yenye mafungamano na Iran huku Tehran nayo ikiapa kuendelea kuufunga Mlango Bahari wa Hormuz

Hapo jana Iran ilionesha ubavu wake wa kijeshi kwa kuchapisha video ya makomandoo wake wakiikamata meli moja ya mafuta karibu na Mlango huo wa bahari huku viongozi wakuu wa nchi hiyo wakipuuzilia mbali madai ya Rais Trump kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye safu ya juu ya utawala wa nchi hiyo.

Hadi sasa bado hakuna ishara ya suluhu ya kudumu kati ya Washington na Tehran kuhusu hatma ya Mlango Bahari wa Hormuz unaopitisha karibu asilimia 20 ya mafuta na gesi duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW