Mvutano mwengine kuhusu Ukuta wa Israel
29 Novemba 2003Matangazo
RAMALLAH: Waziri Mkuu wa Kipalestina, Ahmed Korei amesisitiza kuwa ule Ukuta unaoigawa Israel na Mamlaka yaliyokaliwa ya Kipalestina ni kizingiti kikubwa kwa juhudi za amani ya Mashariki ya Kati. Akiwahutubia waandishi wa habari mjini Ramallah, Bwana Korei alitishia kuvunja ile mipango yake ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel, Ariel Sharon, ikiwa kiongozi huyo hayuko tayari kuwaridhia Wapalestina katika maswali kadha muhimu yanayoleta ubishi. Hata hivyo, kwa hivi sasa yanaendelezwa maandalizi ya mkutano huo, alisema Bwana Korei. Upande wake, Israel imepinga yale mashtaka ya Katibu Mkuu wa UM, Kofi Annan kuwa Israel imeezeka ukuta wake mpaka ndani ya ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mashtaka ya Bwana Annan kwamba Israel inavunja sheria za kimataifa kwa Ukuta wake huo, ni tuzo kwa wote wale wanaofuatiliza shabaha zao kwa harakati za kigaidi, ilisema taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel.
