1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa Marekani, Israel na Iran watikisa UN

1 Machi 2026

Katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani na Israel zimejikuta zikikabiliana vikali na Iran, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa wito wa kusitisha mashambulizi.

New York 2026 | Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanakiuka sheria za kimataifa.Picha: Heather Khalifa/REUTERS

Guterres aliliambia baraza hilo kwamba lazima juhudi ziongezwe kuzuia kuongezeka kwa mzozo, akionya kuwa kushindwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha vita pana vyenye madhara makubwa kwa raia na utulivu wa kikanda.

Aidha Guterres amesema mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanakiuka sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa,  na amekosoa mashambulizi ya Iran yalioibuka kama majibu yake yenye kushindwa kuheshimu uhuru wa nchi nyingine.

Marekani kupitia balozi wake Mike Waltz, ilitetea hatua zake, na kuzitaja kuwa halali na muhimu katika kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia. Israel pia ilisema mashambulizi yake ni ya kujilinda dhidi ya tishio la kimaangamizi.

Kwa upande mwingine, balozi wa Iran aliitaka dunia ikusanye nguvu kutoa mwongozo wa amani badala ya njia za kijeshi, akisema mashambulizi hayo yameua na kujeruhi mamia ya raia na kuyataja kama uhalifu wa vita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW