1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Mvutano waongezeka kati ya Durtete na kiongozi wa Ufilipino

29 Januari 2024

Nchini Ufilipino mvutano unaongezeka kati ya familia ya rais wa zamani Rodrigo Durtete na kiongoni mpya Ferdinand Marcos Jr.

19.04.2018 Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte akiwafanyia utani wapiga picha baada ya kushikilia bunduki aliyokabidhibiwa na mkuu wa polisi.
19.04.2018 Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte akiwafanyia utani wapiga picha baada ya kushikilia bunduki aliyokabidhibiwa na mkuu wa polisi. Picha: Bullit Marquez/AP Photo/picture alliance

Jana Jumapili, mtoto wa kiume wa Durtete alimtaka Rais Marcos Jr ajiuzulu akimuita ni mtu mvivu na asiyewajali wengine.

Sebastian Durtete ambaye ni meya wa mji wa tatu wenye idadi kubwa ya watu nchini humo wa Davao amesema kuna ongezeko la visa vya uhalifu baada ya kampeini ya kukabiliana na madawa ya kulevya iliyoanzishwa na baba yake kusitishwa.

Meya huyo pia amemshutumu rais Marcos Jr kwa kuruhusu ujenzi wa kambi za kijeshi za Marekani nchini humo ikiwemo karibu na kisiwa cha Taiwan.

Rais wa zamani Durtete alikuwa karibu zaidi na China.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW