1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano waongezeka Msumbiji kabla ya idhini ya matokeo

23 Desemba 2024

Msumbiji inajiandaa kupitishwa hii leo Jumatatu huku kiongozi wa upinzani akiapa kuendeleza "vurumai" ikiwa chama tawala kitathibitishwa kuwa mshindi katikati ya mzozo ambao tayari umegharimu maisha ya watu 130.

Mosambik Parlamentswahl I Stimmung nach Verkündung des Wahlergebnisses in Maputo
Hali ilivyo kabla ya kuidhinisha matokeo ya uchaguzi huko MaputoPicha: Romeu da Silva/DW

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imekumbwa na machafuko tangu tume ya uchaguzi ilipotangaza kuwa mgombea wa chama tawala cha Frelimo,Daniel Chapo ambacho kimeshika madaraka tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975 ameshinda katika uchaguzi wa Oktoba 9. Baraza la Katiba linatarajiwa kuyaidhinisha matokeo hayo ya ushindi wa FRELIMO mwendo wa saa tisa alasiri kwa saa za Msumbiji. Daniel Chapo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Rais Filipe Nysui ambaye muhula wake wa pili unamalizika Januari 15. Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane anadai kura ziliibiwa na kwamba yeye na wafuasi wake wataendeleza maandamano ya kupinga matokeo hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW