Upo usemi wa Kiswahili usemao, mkuki kwenda porini, ndio mahali pake. Hilo linathibitishwa ya familia ya watoto kumi na nane wa familia moja wanaojihusisha na kazi ya upigaji wa muziki kwa kutumia vyombo asilia nchini Tanzania na kujipatia umaarufu na kufanya kazi hizo kwenye mataifa mbalimbali duniani.