1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka 2024 kuwa mwaka wenye joto zaidi

9 Desemba 2024

Shirika la ufuatiliaji mabadiliko ya tabianchi la Umoja wa Ulaya, Copernicus, limesema kuwa ni hakika mwaka huu utakuwa wa joto zaidi kurekodiwa na wa kwanza uliopita kiwango muhimu cha kulinda dunia dhidi ya joto kali.

Vanuatu Port Vila 2019 | Küstenlinie im Kontext des steigenden Meeresspiegels und der Folgen von Zyklon Pam
Picha: Mario Tama/Getty Images

Kiwango hicho kipya kilichothibitishwa na shirika hilo la Copernicus, kinahitimisha mwaka ambapo nchi tajiri na maskini zilikumbwa na majanga ambayo wanasayansi wamehusisha na shughuli za binadamu katika ongezeko la kasi la joto duniani.

Copernicus inasema, hali ya joto isiyo ya kawaida iliongeza kiwango cha wastani cha halijoto duniani kati ya Januari na Novemba hivi kwamba mwaka huu ulikuwa na uhakika wa kuwa na viwango vya juu vya joto visivyo vya kawaida.

Katika hatua nyingine mbaya, 2024 utakuwa mwaka wa kwanza wa joto la zaidi ya nyuzi 1.5 kuliko nyakati za kabla ya viwanda kabla ya wanadamu kuanza kuchoma kiasi kikubwa cha nishati ya visukuku.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW