1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka 1 baada ya mapinduzi ya Sudan, Je kuna lililofanikiwa?

Oumilkheir Hamidou
19 Desemba 2019

Kupinduliwa mtawala wa muda mrefu Sudan Omar al-Bashir ndio uliokuwa mwanzo wa kipindi cha mpito kuelekea demokrasia nchini Sudan. Lakini mzozo wa kiuchumi na wadau kadhaa wa kijeshi wanatishia kuyapindua mapinduzi

Sudan Khartum | Prozess & Urteil Omar al-Baschir, ehemaliger Präsident | Anhänger
Picha: Getty Images/AFP/A. Shazly

Takriban mwaka mmoja tangu wimbi la malalamiko dhidi ya kupanda bei ya mkate na mafuta kugeuka miito kumtaka mtawala wa muda mrefu wa Sudan Omar al-Bashir ang'atuke, mapinduzi ya Sudan yaliwafanya watu wawe na matumaini.

Maandamano ya decemba 2018 yalichchea mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'owa madarakani al Bashir mwezi wa April. Hadi wakati huo mtawala huyo wa kimabavu, al Bashir alionekana kana kwamba hakuna hadhoofiki, akiwatia jela wapinzani, akikandamiza maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wake na kuamuru maatumizi ya nguvu na umwagaji damu katika maeneo ya kusini na magharibi mwa nchi yake katika kipindi cha miaka 30 ya utawala wake.

Kipindi cha utawala wa muimla huyo aliyefikiri hashindiki kilimalizika jumamosi iliyopita alipokutikana na hatia ya kuhusika na rushwa mahakamani. Hata hivyo makubaliano yaliyofikiwa kwaajili ya kipindi cha mpito kuelekea mfumo imara wa kidemokrasi bado ni dhaifu.

Vuguvugu la maandamano ambalo kwa sehemu kubwa lilikuwa la amani lilikuwa kilele cha muundo wa taasisi za akiraia na upinzani chini ya utawala wa al Bashir.tangu alipong'olewa madarakani, hatua za kutia moyo zimechomoza.

"Si kitu chengine isipokuwa mageuzi ya kina katika utambulisho wa wasaudan,taasisi na jamii," anaasema mtaalam wa mauala ya sudan Jonas Horner wa shirika la kimataifa linalochunguza mizozo,katika mahojiano na DW.

Baraza la raia na wanajeshi  laundwa kusimamia kipindi cha mpito cha miaka mitatu

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok Picha: Getty Images/AFP/E. Hamid

Licha ya mauwaji yaliyofanywa na wanamgambo wa vikosi vya kuingilia kati haraka waliowaauwa watu 100 mwezi Juni uliopita,upande wa upinzani-muungano wa makundi yanayopigania uhuru na mageuzi yamefanikiwa kuunda baraza la raia na wanajeshi miezi miwili baadae ili kusimamia kipindi cha mpito cha miaka mitatu kabla ya uchaguzi kuitishwa.

Kuteuliwa waziri mkuu Abdallah Hamdok mwezi wa Agosti, mtaalam wa kiuchumi anaeheshimika pamoja pia na baraza la mawaziri wa serikali ya mpito mwezi wa septemba ilikuwa hatua muhimu iliyoleta mataumaini hatua zaidi zitachukuliwa kuinua haali ya kiuchumi ambayo ndio chanzo cha maandamano ya amwaka jana.

Kuibadilisha sura ambaya ya Sudan kama dola lililotengwa na jamii ni jambo la maana pia katika kuipatia sudan misaada ya kiuchumi. Na ziara aliyoifanya waziri mkuu hamdok mapema mwezi huu wa decemba mjini Washingon ikapelekea kuteuliwa balozi wa Marekani mjini Khartoum kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23.

Serikalai ya waziri mkuu Hamdok imeangaza hivi karibuni orodha ya hatua 10 muhimu ikiwa ni pamaoja na zilee za kuupatia aufumbuzi mzozo wa kiuchumi,mapambano dhidi ya rusdhwa na kumaliza mizizozo yaq muda mrefu iaoizonga nchi hiyo. Wadadisi wanaona kuna matumaini ya kufikiwa amani pamoja na makaundi ya waasi .

Chanzo: Allinson,Thomas

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW