1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mwaka mmoja wa Taliban madarakani

15 Agosti 2022

Tangu Taliban walipotwaa kwa nguvu madaraka nchini Afghanistan baada ya wanajeshi wa NATO na Marekani kuondoka hali ya maisha ya Waafghani imebadilika na kuwa ngumu zaidi

Afghanistan | Frauenrechte | Proteste in Afghanistan
Picha: Wakil Kohsar/AFP

Kundi la Taliban leo limetimza mwaka mmoja tangu lilipotwaa madaraka nchini Afghanistan. Taliban waliiushangaza ulimwengu kwa kuudhibiti ghafla mji mkuu Kabul mnamo mwaka jana Agosti 15 baada ya jeshi la Marekani na vikosi vya jumuiya ya kujihami Nato kuondoka.Vikosi vya serikali iliyokuwepo wakati huo ikiongozwa na rais Ashraf Ghani,vilishindwa kuwazuia Taliban. Je maisha yamebadilika kwa kiasi gani katika nchi hiyo?

Mwaka Jana tarehe kama ya Leo hatimae kundi lenye misimamo mikali ya kiislamu la Taliban lilifanikiwa kurudi tena madarakani baada ya utawala wao kuondolewa madarakani kwa nguvu  mnamo mwaka 2001 na Marekani kupitia uvamizi wa kijeshi. Wataalamu wanasema kuporomoka kwa serikali ya Ashraf Ghani lilikuwa jambo lisiloweza kuepukika pale tu jumuiya ya kujihami ya NATO ilipoanza kuondowa wanajeshi wake katika nchi hiyo mnamo mwezi Mei mwaka 2021.

Hatua ya kuondoka wanajeshi hao ilitokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na kundi hilo la Taliban Februari mwaka 2020. Lakini ni wachache waliotarajia nchi hiyo ya Afghanistan itaangukia mikononi mwa wanamgambo hao haraka kama ilivyotokea. Mbali ya athari za kisiasa za kikanda kutokana na kurudi madarakani kwa Taliban,maisha ya wafghanistan wakawaida yamebadilika kwa kiwango kikubwa tangu mwaka jana,na kwa wengi maisha yamezidi kuwa magumu.

Picha: DW

Licha ya kusikika sauti za kuzikosoa serikali zilizopita nchini Afghanistan zilizoungwa mkono na Marekani baada ya kuwaondoa Taliban mwaka 2001,nchini hiyo ya Afghanistan ilikuwa imepiga hatua katika maeneo mengi katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Vyombo huru vya habari viliimarika chini ya utawala wa rais  Hamid Karzai na vile vile chini ya utawala wa rais Ashraf Ghani.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalishuhudia hatua ikipigwa,idadi ya wasichana walioanza shule na vyuo vikuu iliongezeka wakati ambapo jamii ya watu wanaoishi maisha ya uchumi wa kati ikionesha kupata maendeleo kiasi katika kipindi hicho hicho. Lakini katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwa kiasi kikubwa  hali hiyo imebadilika. Saleha Ainy, ni mwandishi habari wa kiafghanistan aliyekimbilia Iran:

Picha: Zerah Oriane/ABACA/picture alliance

"Taliban walijaribu kunikamata mara kadhaa.Walikuja nyumbani kwetu mara nyingi.Na walipotoa onyo kwa familia yangu basi sikuwa na budi bali kuondoka Afghanistan.

Kundi la Taliban limeshindwa kutimiza nyingi ya ahadi zao chini ya makubaliano yaliyofikiwa mjini Doha huko Qatar mwaka 2020. Kundi hilo limeshindwa kuunda serikali shirikisho katika taifa hilo wakati wasichana walioko madarasa ya juu wakizuiwa kwenda shule na wanawake wakinyimwa fursa ya kufanya kazi katika sekta nyingi au hata kutembea peke yake kwenda  kwenye maeneo ya bustani za kupumzika.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW