1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mwaka mmoja wa vita Sudan: Hali inazidi kuwa mbaya zaidi

15 Aprili 2024

Umoja wa Mataifa umesema mwaka mmoja wa vita vya Sudan kati ya majenerali hasimu nchini humo umesababisha maafa makubwa, mamilioni ya watu wakiyakimbia makazi yao huku wakikabiliwa na njaa na madhila mengine

 Sudan
Picha ya mzee na raia wa Sudan akiwa kwenye tafakari katika eneo yanakoendelea mapigano Picha: AFP/Getty Images

Umoja wa Mataifa umesema mwaka mmoja wa vita vya Sudan kati ya majenerali hasimu nchini humo umesababisha maafa makubwa, mamilioni ya watu wakiyakimbia makazi yao huku wakikabiliwa na njaa na madhila mengine chungu nzima. Ripoti ya umoja wa Mataifa inasema upande wa kaskazini wa nchi hiyo ndio umeathirika zaidi na ndiko yanakoshuhudiwa maafa mabaya zaidi ya kibinadamu.

Soma zaidi.Wakimbizi wa Sudan wateseka Sudan Kusini 

Kwa mujibu wa  msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni,WHO, Christian Lindmeier akizungumza mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva amesema bila kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan hali inaweza kuwa mbaya  zaidi kwa siku zijazo na pia upo uwezekano kwamba athari zake zikasambaa hata kwa mataifa jirani.

Shirika la afya Duniani WHO limeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi nchini sudan kama vita vitaendeleaPicha: David Allignon/MAXPPP/dpa/picture alliance

Vita hivyo ambavyo vinatimiza mwaka mmoja tangu vilipozuka vimesababisha mamilioni ya wasudan kuwa wakimbizi huku wakikakabiliwa na ukosefu wa huduma za kimsingi ikiwemo chakula,  kuharibika kwa miundombinu na kuenea kwa magonjwa ni miogoni mwa madhila wanayokumbana nayo kila siku.

Soma zaidi. Watu 12 wauawa katika shambulizi la droni nchini Sudan

Shirika la Afya Duniani linaeleza kuwa vita hivyo vimewaua maelfu ya watu na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu, Zaidi ya watu milioni 8.5 wamekimbia makazi yao, huku karibu milioni 1.8 wakivuka mipaka ya nchi hiyo kwenda kwenye mataifa mengine.

WHO yaendelea kutoa onyo kwa jumuiya ya kimataifa

WHO imeonya kuhusu kudorora kwa mfumo wa afya, uhaba wa wafanyakazi. dawam, chanjo  na vifaa vya afya,  asilimia 70 hadi 80 ya vituo vya afya vya Sudan havifanyi kazi kutokana na mapigano hayo yanayoendelea.

Balozi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield amesema wakati jamii zikukubana na njaa, magonjwa nayo yanazidi kuhatarisha usalama wa maisha yao.

"Wakati jamii zikikabiliana na njaa, ugonjwa wa kipindupindu na surua unazidi  kuenea, huku ghasia zikiendelea kugharimu maisha ya watu wengi, dunia kwa kiasi kikubwa imekaa kimya, na hilo lazima libadilike. Na lazima libadilike sasa. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa zaidi. Ni lazima kufanya hivyo. zaidi. Na inapaswa kujali zaidi."amesema balozi huyo.

Balozi wa kudumu wa Marekani kwenye baraza la Umoja wa Mataifa amesema hatua zinapaswa kuchukuliwa haraka kuwasaidia raia wa SudanPicha: Yuki Iwamura/AP/picture alliance

Soma zaidi. Shule zitafunguliwa tena Sudan Kusini baada ya wiki mbili za joto kali

Kwa sasa vikosi vya Shule zitafunguliwa tena Sudan Kusini baada ya wiki mbili za joto kali serikali nchini Sudan vinatumia nguvu kubwa ya mashambulizi ya anga kuyarudisha maeneo ambayo yamechukuliwa na kikosi cha  RSF ingawa upo ukosoaji kwamba jeshi hilo limeshindwa kuwalinda raia wakati wa mashambulizi yake.

Utafiti wa Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa mwaka 2024 utakuwa mwaka wa njaa zaidi nchini  Sudan hasa katika miji ya Darfur na Kordofan na hiyo ni kutokana na kupoungua kwa uzalishaji na mfumuko mkubwa wa bei. 

Kongamano la kimataifa la kibinadamu kwa ajili ya  Sudan likiongozwa na Ufaransa liaandaa mkutano mjini Paris wa kujadili namna ya kuongeza ufadhili huku asilimia sita tu ya makadirio ya dola bilioni 2.7 zinazohitajika kushughulikia mzozo huo zikiwa zimekusanywa hadi sasa.