1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mwanadiplomasia wa Ufaransa ahimiza utulivu Lebanon

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Mwanadiplomasia mkuu wa Ufaransa Stephane Sejourne, ametoa wito wa utulivu nchini Lebanon wakati wa ziara yake ya pili tangu kulipozuka mvutano wa mashambulizi ya kuvuka mpaka na Israel yaliyochochewa na vita vya Gaza.

Mwanadiplomasia mkuu wa Ufaransa Stephane Sejourne(katikati) alipokutana na Spika wa Lebanon Nabih Berri(kulia)
Mwanadiplomasia mkuu wa Ufaransa Stephane Sejourne(katikati) alipokutana na Spika wa Lebanon Nabih Berri(kulia)Picha: Hassan Ammar/AP Photo/picture alliance

Mwanadiplomasia mkuu wa Ufaransa Stephane Sejourne, ametoa wito wa utulivu nchini Lebanon wakati wa ziara yake ya pili tangu kulipozuka mvutano wa mashambulizi ya kuvuka mpaka na Israel yaliyochochewa na vita vya Gaza.

Sejourne alitembelea makao makuu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon UNFIL na kusisitiza kwamba Paris inahimiza uepushaji vita nchini humo.

Israel na kundi la Hezbollah la nchini Lebanon linaloungwa mkono na Iran, zimekuwa zikishambuliana kwa kufyatiliana risasi karibu kila siku tangu shambulizi la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7.

Mapigano yameongezeka katika wiki za hivi karibuni, huku Israel ikipiga hatua zaidi ndani ya ardhi ya Lebanon, huku Hezbollah ikiongeza mashambulizi yake ya makombora na ndege zisizo na rubani kwenye maeneo ya kijeshi kaskazini mwa Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW