1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia wa Urusi Lavrov ahitimisha ziara yake Afrika

6 Juni 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amehitimisha ziara yake ya siku tano barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov
Urusi inaendelea kutafuta ushawishi katika bara la Afrika wakati ikiendelea kutengwa na nchi za MagharibiPicha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Katika ziara hiyo, Lavrovaliendelea kuzinyooshea kidole nchi za Magharibi katika suala la vita vya Ukraine, huku akielezea azma ya nchi yake kukaribiana zaidi na Chad.

Soma pia: Lavrov aanza ziara Afrika kwa kuitembelea Guinea

Kwenye mkutano na waandishi habari mjini Ndjamena baada ya mazungumzo na Rais Mahamat Deby Itno, Lavrov amesema Urusi iko tayari kushirikana na Chad katika sekta nyingi lakini ni Wachad wenyewe watakaoweka wazi orodha ya mahitaji yao.

Lavrov aliongeza kuwa urafiki wa Urusi na Chad hautaathiri uhusiano wa nchi hiyo ya Sahel na Ufaransa.

Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Chad, Adberaman Koullamalah, amesema kwamba

Chad ni nchi huru, inakuza na kudumisha uhusiano na yeyote inayomtaka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW