1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Bernardo Arevalo ashinda urais wa Guatemala

21 Agosti 2023

Mwanaharakati wa kupambana na rushwa, Bernardo Arevalo, ameshinda uchaguzi wa rais nchini Guatemala baada ya kuchaguliwa kwa asilimia 58 ya kura.

Guatemala | Anti-Korruptions-Präsidentschaftskandidat Bernardo Arevalo
Picha: Pilar Olivares/Reuters

Ushindi huo ameupata dhidi ya mpinzani wake aliyekuwa mke wa rais wa zamani, Sandra Torres, aliyepata asilimia 37, kwa mujibu wa matokeo ya awali. Arevalo, mwenye umri wa miaka 64, aliwahi kuwa mwanadiplomasia na mtoto wa rais wa zamani ameahidi kuziondowa taasisi zilizotawaliwa na rushwa na kuwahimiza watu kujishughulisha na kile alichokiita mapambano ya kupigania haki kurejea nchini Guatemala baada ya kushuhudiwa visa kadhaa vya kuikimbia nchi waendesha mashataka, majaji na waandishi habari.Ushindi wa Aravelo umekuja wakati machafuko na ukosefu wa usalama wa chakula vikiikabili nchi hiyo na kusababisha wimbi la watu kuihama nchi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW