Mwanaharakati mshindi mbadala wa Tuzo ya Nobel
1 Oktoba 2020Matangazo
Ales na shirika la haki za binadamu aliloasisi liitwalo Viasna wametambuliwa kwa mchango mkubwa wa kudai demokrasia na haki za binadamu nchini Belarus, ambako kwa wiki kadhaa waandamanaji wanapinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Agosti.
Mshindi mwingine wa tuzo hiyo ni mwanasheria kutoka Iran Nasrin Sotoudeh aliyewatetea wanaharakati, wanasiasa wa upinzani na wanawake walioshtakiwa kwa kosa la kutovaa hijab.
Washindi wengine wawili wa tuzo hiyo ni mwanasheria wa haki za kiraia wa nchini Marekani Bryan Stevenson pamoja na mwanaharakati wa masuala ya mazingira kutoka nchini Nicaragua Lottie Wren.