1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa Tanzania atekwa kabla ya kuokolewa Kenya

24 Februari 2026

Shirika la Kimataifa la Haki za Binaadamu - Amnesty International limesema kuwa mwanaharakati mmoja wa haki za binaadamu kutoka Tanzania alitekwa nyara nchini Kenya lakini akanaokolewa kabla ya kurejeshwa nyumbani.

Nembo ya Amnesty International
Shirika la Amnesty International limesema mwanaharakati wa Tanzania alitekwa nyara lakini akaokolewa KenyaPicha: Pond5 Images/IMAGO

Mshabaha Mshabaha Hamza amekuwa mmoja wa wakosoaji wakuu wa ukandamizaji mkali dhidi ya maandamano uliofanywa na vikosi vya usalama vya Tanzania wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Amnesty ilisema katika taarifa kuwa Hamza, ambaye amekuwa uhamishoni nchini Kenya kwa takriban miaka minne, alikamatwa na kuingizwa kwenye gari Jumapili iliyopita na wanaume watatu. Hamza alipambana na watekaji hao na akatupwa "akiwa amepoteza fahamu kutokana na madawa aliyopewa na kujeruhiwa" huko Lukenya katika kaunti ya Machakos.

Polisi walijibu "mara moja", na kukamata gari lililotumiwa na watekaji nyara hao -- Wakenya wawili na Mtanzania mmoja. Amnesty imeliambia shirika la habari la AFP kwamba washukiwa hao walikuwa wameahidiwa malipo ya kumpeleka Hamza kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania. Waziri wa habari wa Tanzania hakujibu ombi la kumtaka azungumzie taarifa hiyo. Aidha polisi na wizara ya mambo ya ndani ya Kenya hawakujibu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW