1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa Tanzania atunukiwa tuzo Ujerumani

11 Desemba 2023

Mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binaadamu kutoka Tanzania, Joseph Moses Oleshangay, ametunukiwa Tuzo ya Haki za Binaadamu ya mji wa Weimar nchini Ujerumani.

Maandamano ya jamii ya Wamaasai katika eneo la Ngorongoro.
Maandamano ya jamii ya Wamaasai katika eneo la Ngorongoro.Picha: Deinis Olushangai

Katika sherehe zilizofanyika jioni ya Jumapili (Disemba 10) mjini Weimar, Oleshangay alikabidhiwa tuzo hiyo yenye thamani ya euro 5,000 kwa kile ambacho watayarishaji walisema ni mchango wake kwenye kupigania haki za jamii ya Maasai.

Kamatakamata ya raia Ngorongoro

This browser does not support the audio element.

Oleshangay, ambaye mwenyewe ni kutoka kabila la Maasai, ni mjumbe wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu na amekuwa akitowa ushauri wa kisheria na kuweka kumbukumbu ya uvunjwaji wa haki za binaadamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mji wa Weimar umekuwa ukitowa tuzo hiyo ya haki za binaadamu kila tarehe 10 Disemba tangu mwaka 1995, ikiwa alama ya wajibu wake kufuatia uhalifu wa utawala wa Kinazi wa Ujerumani.