1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Halaiki yaua mwanajeshi mmoja aliyedhaniwa kuwa M23

11 Novemba 2023

Mwanajeshi mmoja ameuwawa kwa kushambuliwa na halaiki huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baadha watu kudhani ni mpiganaji wa kundi la waasi wa M23.

Waasi wa M23
Waasi wa M23Picha: GLODY MURHABAZI/AFP via Getty Images

Hayo yamefahamishwa na duru kadhaa za habari kwenye eneo ambalo linashuhudia wimbi la machafuko yanayotokana na mapigano kati ya jeshi la taifa na waasi wa M23. 

Hii leo jeshi la Kongo limesema Kanali Rutasura Gasore aliuwawa Alhamisi jioni kwenye mji wa Goma bila ya kutoa maelezo ya ziada.

Soma zaidi: DRC: Waasi wa M-23 kuuzingira mji wa Goma

Lakini vyanzo kadhaa vilivyonukuliwa na shirika la habari la AFP vimesema afisa huyo wa jeshi alipoteza maisha baada ya kushambuliwa na wakaazi wa eneo alilokuwa akiishi waliodhani ni mpiganaji wa kundi la M23.

Jeshi limesema tayati limefungua uchunguzi kuhusiana na mazingira ya kifo cha mwanajeshi huyo na limewakamata washukiwa wawili kwa mahojiano.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW