Mwanajeshi mmoja na wanamgambo wanne wauwawa Kongo
12 Mei 2023Matangazo
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa jeshi la Kongo ambalo limesema kundi la wapiganaji linalofahamika kama "Mobondo" ndiyo limehusika na shambulizi hilo. Msemaji wa jeshi la Kongo Sylvain Ekenge amesema kundi hilo lilikivamia kijiji cha Nguma Alfajiri ya jana Alhamisi na katika mapambano yalitokea mwanajeshi mmoja alipoteza maisha kutokana na majeraha.
Soma zaidi:DRC: Mauaji dhidi ya raia yanaendelea licha ya uwepo wa vikosi vya usalama
Kundi la Mobondo linahusishwa na jamii iitwayo Yaka ambayo imo kwenye mzozo wa kuwania hatimiliki za ardhi na kabila lingine la Teke. Mapigano kati ya jamii hizo yamekuwa yakiripotiwa zaidi kwenye jimbo la Mai-Ndombe na ikadiriwa zaidi ya watu 300 wameuwawa tangu mwezi Juni mwaka jana.