Mwanajeshi wa Italy auwawa Afghanistan
24 Novemba 2007Matangazo
Mwanajeshi mmoja wa Italy amekufa kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha kuwashambulia wanajeshi wa Italy wanaojenga daraja yapata kilomita 10 magharibi mwa mji mkuu, Kabul.
Mshambuliaji huyo alitaka kuwaua wanajeshi hao lakini akawaua wanafunzi sita wa shule. Maafisa wa Afghanistan wanasema watu 12 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo, wakiwemo wahandisi watatu kutoka Italy.