1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa kuweka amani wa kikosi cha Umoja wa Afrika auwawa Mogadishu

Othman, Miraji1 Agosti 2008

Mwanajeshi wa kutoka Uganda auwawa Somalia

Mwanajeshi wa kuweka amani kutoka Uganda akipiga doria katika kiwanja cha ndege cha MogadishuPicha: AP

Mwanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika, AU, kinacholinda amani nchini somalia aliuliwa leo pale mripuko wa bomu lililokua karibu na barabara ulipoupiga mlolongo wa magari katika mji mkuu wa Mogadishu.

Mwanajeshi huyo anatokea Uganda. Mlolongo huo wa magari sita ulikua unatokea Uwanja wa Ndege pale ulipolengewa na bomu lililotegwa pembezoni mwa barabara. Mmoja wa wanajeshi wa jeshi la Umoja wa Afrika la kulinda amani alikufa katika shambulio hilo. Mashahidi kadhaa walihakikisha kwamba shambulio hilo lilitokea katika barabara nyembamba zinazolindwa vikali katika mji mkuu huo wa Somalia. Moja ya magari yaliokuwa katika mlolongo huo liliharibika kabisa, lakini haijulikani watu wangapi waliumia.

Hivi sasa Umoja wa Afrika, AU, una wanajeshi 2,600 wa kuweka amani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika, kikosi ambacho ni kidogo na kile cha 8,000 ambacho kiliahidiwa kutolewa na umoja huo. Uganda ilikua nchi ya kwanza kukubali kuchangia na Burundi ikapeleka kikosi chake mwanzoni mwa mwaka huu.

Mapatano ya kusitisha mapigano yalifikiwa mwezi Juni baina ya serekali ya mpito inayoungwa mkono na Ethiopia na vuguvugu kubwa la siasa za Kiislamu katika nchi hiyo. Mapatano hayo yamepelekea mgawanyiko miongoni mwa wapinzani, huku wale wenye siasa kali wakishikilia wanajeshi wa Ethiopia walioivamia nchi hiyo tangu mwaka 2006 lazima waondoke kabla ya kuanza kufanyika mazungumzo ya amani.

Na kabla ya kuja studioni nimeweza kuwasiliana na Meja Bahuko Barije wa jeshi la Uganda ambaye ni msemaji wa jeshi la Umoja wa Afrika linaloweka amani huko Somalia, na akanielezea hivi juu ya mkasa huo wa leo wa huko Magadishu:


Insert: Interview Othman/ Barije...




Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW