1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mwanajeshi wa pili wa kulinda amani Mali, afariki

13 Juni 2023

Mwanajeshi wa pili wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati yalipotokea mashambulizi kaskazini mwa Mali katika eneo la Timbuktu.

Mwanajeshi wa kulinda amani wa Senegal, akiwa amesimama karibu na gari la Umoja huo katika kijiji cha Ogossagou, Mopti nchini Mali, Novemba 5, 2021.
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi katika mataifa mbalimbali.Picha: Amaury Hauchard/AFP/Getty Images

Hujuma hiyo ilifanywa siku ya ijumaa, ambapo kifaa cha kienyeji cha mripuko kilirushwa kuwalenga walinda usalama na baadaye zilitumika silaha ndogo ndogo kushambulia kilomita saba kutoka kambi yao iliyoko mji wa Ber na mlinda amani mmoja aliuwawa na wengine wanane walijeruhiwa vibaya. Wanajeshi wote hao wa Minusma, walioshambuliwa ni raia wa Burkina Faso.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na baraza la usalama la Umoja huo wamelaani mashambulio hayo na kuzitaka mamlaka nchini Mali kuwatafuta waliofanya hujuma hizo na kuwachukulia sheria,Umoja huo ukisema kwamba mashambulizi dhidi ya walinda amani wa taasisi hiyo huenda ukaatazamwa kama uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa.