1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa Uganda ahukumiwa kifungo cha maisha jela

9 Desemba 2021

Mahakama ya jeshi nchini Uganda imemhukumu kifungo cha maisha mwanajeshi aliyepatikana na hatia ya kufanya mauaji ya kukusudia wakati wa ghasia za mwezi Novemba mwaka 2020.

Uganda EU AMISOM Friedenstruppe
Picha: DW/E. Lubega

Mwanajeshi mwingine amehukumiwa kifungo cha miaka 35 kwa hatia hiyo hiyo na mahakama hiyo.

Hukumu hizo zinakuja siku moja baada ya serikali ya Marekani kumwekea vikwazo vya kifedha mkuu wa ujasusi katika jeshi kwa madai kuwa alihusika moja kwa moja katika vifo vilivyotokea katika ghasia hizo ambapo watu zaidi ya 50 walipoteza maisha yao.

Ghasia hizo zilifuatia kukamatwa kwa aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi alipokuwa akifanya kampeni mashariki mwa Uganda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW