Upendosia Peter Moshi ni mwalimu wa shule ya awali ambaye amejikita kuwafundisha watoto waliolazwa wodini kwa kipindi kirefu na wanaougua maradhi sugu yakiwemo saratani. Ana shauku ya kuona watoto wanapata elimu bila kujali changamoto wanazopitia na kuwafanya wazazi kutopoteza tumaini kuhusu hatma za watoto wao.