1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamuziki Oliver Mtukudzi amefariki dunia

23 Januari 2019

Mwanamuziki maarufu nchini Zimbabwe, Oliver Mtukudzi amefariki dunia leo baada ya kuugua ugonjwa wa kisukari.

Zimbabwe Harare International Festival of Arts (HIFA)
Oliver Mtukudzi (kulia) akiwa na mwanamuziki wa Mali, Habib Koite (kushoto)Picha: DW/P. Musvanhiri

Mtukudzi aliyekuwa mashuhuri ulimwenguni kote amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66.

Katika kazi yake ya muziki Oliver aliyejulikana kama 'Tuku' alitengeneza albamu 67 zilizokuwa na nyimbo kadhaa ambazo zilisambaza umaarufu wake katika bara la Afrika na duniani kote kwa ujumla.

Mtukudzi ameimba nyimba na wanamuziki nguli barani Afrika akiwemo marehemu Hugh Masekela, aliyejulikana kama 'Baba wa muziki wa Jazz nchini Afrika Kusini. Pia amewahi kushirikiana na kundi la Afrika Kusini la Black Mambazo.

 

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/AP, Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW