1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanandondi Manny Pacquiao astaafu na kugeukia siasa

29 Septemba 2021

Bondia maarufu wa Ufilipino Manny Pacquiao ametangaza rasmi kustaafu mchezo huo ili kuelekeza nguvu zake katika siasa. Pacquiao ametangaza nia ya kuwania Urais nchini Ufilipino katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Las Vegas WBO Boxen Manny Pacquiao vs Timothy Bradley
Picha: picture-alliance/dpa/M. Nelson

Pacquiao ni bingwa wa mataji mbalimbali duniani katika mchezo wa ndondi amesema hivi; "Ningependa kuwashukuru mashabiki dunia nzima na hasa Wafilipino kwa kuniunga mkono. Kwaheri ndondi", Bondia huyo mwenye umri wa miaka 42 alisema kwenye ujumbe wa video uliyochapishwa katika ukurasa wake wa Facebook.Pacquiao kutupiana makonde na Khan​​​​​​​

"Ni uamuzi mgumu kwangu kukubali kuwa wakati wangu kama bondia umekwisha. Leo natangaza kustaafu."

Pacquiao ambaye amedumu kwenye ulingo wa masumbwi kwa takriban miaka 26 anastaafu baada ya kushiriki mapigano 72 akiibuka mshindi mara 62, na kupoteza mapigano 8.

Bondia huyo ameshinda mataji 12 ya dunia katika mikanda tofauti na ndiye bondia pekee kushikilia ubingwa wa dunia kwa miongo minne.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte na seneta Manny PacquiaoPicha: Getty Images/M.Dejeto

Katika pigano lake la mwisho, Pacquiao alishindwa na bondia wa Cuba Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita.

"Asante kwa kubadilisha maisha yangu. Wakati familia yangu ilikuwa imekata tamaa mulikuwepo kunitia moyo, mulinipa nafasi ya kuboresha maisha yangu", Pacquiao aliwaambia mashabiki wake kupitia ujumbe wa video.

"Kwa ajili yenu nimefanikiwa kuwahamasisha watu ulimwenguni na pia sasa nina nafasi bora na ujasiri wa kubadilisha maisha ya wengi.”

Mapema mwezi huu, bondia huyo ambaye pia ni seneta nchini Ufilipino alikubali uteuzi wa chama chake cha siasa na kutangaza kuwa atawania Urais katika uchaguzi wa Mei mwaka ujao. Ameahidi kupambana na umasikini na kuwaonya wanasiasa fisadi kujitayarisha kwa mapambano wakati wa hatamu yake.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW