1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoAfrika Kusini

Semenya asema uamuzi wa mahakama ya haki ni mwanzo tu

12 Julai 2023

Mwanariadha maarufu wa Afrika Kusini Caster Semenya ameusifu uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Ulaya ambao umehitimisha kuwa haki zake zilikiukwa na mahakama za Uswisi.

Caster Semenya südafrikanische Mittelstreckenläuferin
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Matthews

Mahakama ya Juu ya Uswisi ilikataa rufaa iliyokatwa na Semenya dhidi ya kanuni za Shirikisho la Mbio za Riadha duniani zilizomtaka kutumia dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone iwapo anataka kuendelea kushiriki mashindano. Aina hiyo ya homoni hutengenezwa kwa wingi kwenye miili ya wanaume ikiwa na jukumu la kuimarisha misuli na ubavu.

Soma pia: Semenya ashinda rufaa kushiriki michezo ya dunia

Mahakama ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kuwa uamuzi wa mahakama ya Uswisi haukutenda haki kwa mwanariadha aliye na rikodi ya kushinda mara mbili mbio za mita 800 kwenye michezo ya Olimpiki. Mwenyewe ameutaja uamuzi wa ni kuwa haki iliyotamalaki na amesisitiza hiyo ni hatua ya mwanzo kwenye mapambano yake.

Semenya anayewekwa kwenye kundi la watu wenye "ukuaji wa kimaumbile tofauti na jinsia wazizonazo" anatambulishwa kisheria kama mwanariadha mwanamke.

Amekataa kutumia dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone (Tes-tee-storoon) tangu kanuni za shirikisho la riadha duniani zilipotangazwa mwaka 2018.