1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpinzani wa Uganda Kizza Besigye amepandishwa kizimbani

20 Novemba 2024

Kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya kijeshi mjini Kampala leo baada ya kukamatwa kwa mabavu akiwa taifa jirani la Kenya mwishoni mwa juma lililopita.

Uganda Kizza Besigye Opposition vor Gericht
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea urais mara nne Kizza Besigye afikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkuu wa Barabara ya Buganda mjini Kampala.Picha: Hajarah Nalwadda/AP/picture alliance

Wakali wake Eria Lukwago ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Besigye, mwenye umri wa miaka 68, alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya dola huku akiwa amefungwa pingu mikononi.

Lukwago amesema mwanasiasa huyo amepinga kesi yake mbele ya mahakama ya kijeshi akisema raia wa kawaida na hastahili kushtakiwa kwenye chombo hicho.

Soma pia:Uganda yawatia hatiani kwa "uhaini" wanachama 16 wa upinzani 

Kesi iliahirishwa ndani ya muda mfupi baada ya Besigye kuieleza pia mahakama kwamba hana uwakilishi wa mawakili kutokana na kuzuia kufanya mawasiliano na mtu yeyote.

Taarifa za kukamatwa wake zilitolewa mapema leo na mkew Winnie Byanyima aliyeandika mitandaoni kwa mumewe alitekwa nyara siku ya jumamosi mjini Nairobi.