1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mwanasiasa wa India Baba Siddique auawa kwa kupigwa risasi

13 Oktoba 2024

Mwanasiasa maarufu katika mji mkuu wa kubiashara wa India, Mumbai, ambaye pia alijulikana kwa uhusiano wake wa karibu na ulimwengu wa tasnia ya filamu nchini humo (Bollywood) ameuawa kwa kupigwa risasi.

Mwanasiasa wa India Baba Siddique
Mwanasiasa wa India Baba SiddiquePicha: Satish Bate/Hindustan Times/picture alliance/Sipa USA

Baba Siddique, mwenye umri wa 66, na aliyehawi kuwa waziri katika jimbo la Maharashtra, alipigwa risasi kadhaa kifuani alipokuwa nje ya ofisi ya mwanawe mjini Mumbai jana usiku na alifariki dunia akiwa katika hospitali ya Lilavati jijini humo.

Siddique ambaye kwa miongo kadhaa alihusishwa na  chama cha Indian National Congress alihamia hivi karibuni katika chama cha kikanda ambacho kinatawala Jimbo la Maharashtra linalotarajiwa kufanya uchaguzi mwezi Novemba.

Vyombo vya habari nchini India vimeripoti kuwa washambuliaji wawili wamekamatwa, na polisi bado inawamsaka mwingine mmoja. Washukiwa hao walidai kuwa sehemu ya genge la uhalifu ambalo limetekeleza mauaji mengi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW