Mpinzani wa Tunisia aliye gerezani asitisha mgomo wa kula
2 Desemba 2025
Katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii uliochapishwa na dada yake, wakili Dalila Mssadek, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 57 ameandika matukio mawili ya maandamano ya hivi karibuni ya mashirika ya kiraia yamedhihirisha kuwa "barabara ya kidemokrasia iliyo hai” inatetea haki za wafungwa wa kisiasa, na hivyo anaweza kusitisha mgomo wake wa siku 33. Ben Mbarek, mwanzilishi mwenza wa muungano wa upinzani wa Tunisia uitwao National Salvation Front (FSN), alikuwa miongoni mwa washtakiwa takriban 40, wengi wao wakosoaji wa Rais Kais Saied, waliotiwa jela Ijumaa kwa ‘njama dhidi ya usalama wa taifa'.Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu yamekosoa kesi hiyo, na mashtaka yalijikita zaidi katika madai ya kukutana na wanadiplomasia wa kigeni. Washtakiwa walihukumiwa mwezi Aprili na wiki iliyopita wakapewa vifungo vya hadi miaka 45.