Mwandishi wa habari maarufu wa Pakistani auawa nchini Kenya
24 Oktoba 2022![Pakistanischer Journalist Arshad Sharif](https://static.dw.com/image/63537327_800.webp)
Matangazo
Mwandishi habari maarufu wa Pakistan,Arshad Sharif ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani usiku wa kuamkia leo katika barabara kuu ya Nairobi-Magadi nchini Kenya. Taarifa za awali zinasema Arshad Sharif aliuawawa baada ya yeye na dereva wake kukaidi amri ya kusimamisha gari lao kwenye kizuizi kilichokuwa kimewekwa kukagua magari.