1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi wa habari China afungwa jela kuhusiana na Covid-19

21 Septemba 2025

Mwandishi wa habari wa China ambaye alifungwa jela kwa kuripoti mlipuko wa awali wa COVID-19, amehukumiwa tena adhabu ya kifungo cha miaka minne jela.

China Wuhan 2020 | Mwandishi wa habari Zhang Zhan
Katika picha hii Aprili 11, 2020, Zhang Zhan amesimama nje ya duka wakati wa ziara ya WuhanPicha: Melanie Wang/AP Photo/picture alliance

Mwandishi wa habari wa China ambaye alifungwa jela kwa kuripoti mlipuko wa awali wa COVID-19, amehukumiwa tena adhabu ya kifungo cha miaka minne jela. Katika kesi mpya, mwandishi huyo Zhang Zhan alikamatwa Agosti mwaka 2024 kwa makosa ya kusababisha matatizo, mashtaka yanayotumiwa mara kwa mara na mamlaka kukandamiza upinzani. Shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka RSF, limesema Zhang aliye na umri wa miaka 42 alitiwa mbaroni kufuatia kuripoti kwake juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na serikali ya China. Katika kesi iliyopita, Zhang alishikiliwa Mei mwaka 2020 baada ya kusafiri katika jiji la Wuhan, ambako alirekodi vidio kwa kutumia simu ya mkononi juu ya taharuki ya ugonjwa huo kwenye kitovu cha mlipuko na kuwahoji maafisi namna wanavyoshughulikia hali hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW