1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi wa Habari wa Radio Okapi auwawa mjini Bukavu,DRC

24 Novemba 2008

Nchini Kongo mazishi ya mwandishi mmoja wa habari yanatarajiwa kufanyika hii leo.Didace Namujimbo mwandishi wa habari wa kituo cha redio cha Umoja wa Mataifa Okapi alipigwa risasi hadi kufa Ijumaa iliyopita mjini Bukavu.

Itakumbukwa kuwa ni mara ya pili kwa kitendo cha namna hii kutokea katika kipindi cha miezi 18.Kituo cha redio cha Okapi kilianzishwa kwa minajili ya kuimarisha juhudi za kumaliza vita vinavyozonga Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Ili kupata picha kamili Thelma Mwadzaya alizungumza na Jerome Sekana mwanachama wa chama cha waandishi wa habari wa Kongo UNPC aliye pia msimamizi wa kituo cha redio cha Raga FM.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW