1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mwandishi wa habari wa Rwanda, amefariki ajalini

20 Januari 2023

Mwandishi wa habari wa Rwanda John Williams Ntwali aliyekuwa akiandika habari ambazo zinaikosoa serikali amefariki kwenye ajali.

Flagge von Ruanda
Picha: Carl Court/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa polisi John Williams Ntwali aliyekuwa na umri wa miaka 44 akifanya kazi kama mhariri katika gazeti la Chronicles alifariki kwenye ajali Jumatano ya pikipiki iliyogongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.Polisi imeeleza Ntwali hakuwa na kitambulisho chochote alipopatwa na ajali hiyo na mwili wake ulitambuliwa jana alhamisi baada ya jamaa zake kupewa taarifa. Mwandishi habari huyo amewahi kukamatwa mara kadhaa katika kipindi cha miongo miwili akiwa kwenye tasnia hiyo, alikuwa akimiliki kituo cha Televisheni ya mtandao wa Youtube inayoitwa Pax iliyojipatia sifa ya kuwa kituo pekee kinachothubutu kuikosoa serikali ya Kigali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW