1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi wa Morocco aliyemtuhumu mwanasiasa afungwa jela

12 Novemba 2024

Mwandishi habari wa Morocco Hamid Mahdaoui, aliemtuhumu mwanasiasa mashuhuri nchini humo kwa ufisadi, amehukumiwa adhabu ya kifungo jela.

Pressefreiheit
Picha: Nyein Chan Naing/dpa/picture alliance

Mwezi uliopita mwakilishi wa shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka kanda ya Afrika Kaskazini, Khaled Drareni aliitaja kesi hiyo kuwa ni matumizi mabaya ya mfumo wa haki katika kutisha na kunyamazisha waandishi wa habari.

Mwandishi huyo atatumikia kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitano jela na anatakiwa kulipa faini ya Dola 150,000 baada ya kukutwa na hatia.

Hamid alishitakiwa baada ya malalamiko kutoka kwa waziri wa sheria Abdellatif Ouahbi. Mwandishi huyo alikuwa amechapisha vidio katika tovuti yake ikimtuhumu waziri kwa ufisadi na rushwa, madai ambayo waziri huyo wa sheria aliyakana yote.