1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUholanzi

Mwendesha mashtaka wa ICC achunguzwa kwa unyanyasaji kingono

12 Novemba 2024

Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu, ICC ya mjini The Hague, Päivi Kaukoranta amesema wameanzisha uchunguzi dhidi ya Mwendesha mashtaka mkuu Karim Khan anayetuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono.

 Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, Karim Khan
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya uhalifu ya mjini The Hague, Karim Khan kuchunguzwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingonoPicha: Peter Dejong/REUTERS

Kaukoranta amesema jana Jumatatu kwamba chombo huru kitachunguza madai hayo ili kuhakikisha mchakato huo unakuwa huru, usioegamia upande wowote na wa haki.

Madai hayo yaliibuliwa mwezi Oktoba, lakini muhanga, ambaye ni mtumishi kwenye ofisi ya Khan aliripotiwa kuupinga uchunguzi na hakutaka kuyazungumzia madai hayo, hivyo kufanya uchunguzi huo kusitishwa.

Khan mwenyewe ameyapuuza madai hayo akisema hayana msingi na kuzihakikishia mamlaka kwamba yuko tayari kushirikiana na wachunguzi.