1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC ina hofu kuhusu ghasia nchini Ivory Coast

29 Oktoba 2020

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusu ghasia zilizozuka huko Ivory Coast, akionya kwamba wale wanaochochea moto machafuko watachukuliwa hatua.

Elfenbeinküste Alassane Ouattara
Picha: AFP/L. Marvin

Watu wapatao 30 wameuawa katika machafuko hayo kote nchini humo tangu mwezi Agosti, kabla ya kufanyika uchaguzi, hali inayozua wasiwasi kuwa huenda taifa hilo likatumbukia tena kwenye mgogoro kama uliotokea mwaka 2010-2011 na kusababisha vifo vya watu 3,000.

Ivory Coast inatarajiwa kufanya uchaguzi Oktoba 31, ambapo Rais aliye madarakani Alassane Ouattara atawania muhula wa tatu madarakani huku akikabiliwa na upinzani mkali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW