1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa hati ya kumkamata raia wa Ukraine

14 Agosti 2024

Mwendesha mashtaka mkuu wa Ujerumani ametoa hati ya kuwezesha kumkamata raia wa Ukraine aliyelihujumu bomba la gesi la Nord Stream kwenye bahari ya Baltiki miaka miwili iliyopita.

Nord Stream 2
Mwendesha mashtaka wa Ujerumani atoa hati ya kumkamata raia wa Ukraine aliehujumu bomba la gesiPicha: Jens Büttner/dpa/dpa-Zentralbild/picture alliance

Mtuhumiwa ambaye mara ya mwisho alikuwapo nchini Poland sasa amejificha.

Milipuko kadhaa iliyaharibu mabomba mawili ya kupitishia gesi na kusababisha huduma kusimama mnamo mwaka 2022.

Urusi yataka majibu kutoka Magharibi kuhusiana na milipuko ya Nord Stream

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Ujerumani, raia wengine wawili wa Ukarine pia wanatuhumiwa kuhusika na hujuma hizo.

Watu hao wanatuhumiwa kuwa wapiga mbizi waliotega mabomu kwenye mabomba ya gesi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW