"Mwenyekiti wa benki ku ya dunia si lazma awe Mmarekani"-inasema Australia
27 Mei 2007Matangazo
CANBERRA:
Australia imejiunga na nchi zinazotaka atakaekabidhiwa wadhifa unaoachwa na Paul Wolfowitz kama mwenyekiti wa benki kuu ya dunia,asiwe raia wa Marekani.”Wengine pia wa kutoka nchi nyengine za dunia wanastahiki kukabidhiwa wadhifa huo”-amesema waziri wa fedha wa Australia Peter Costello.Australia inaunga mkono kikamilifu madai ya mataifa 20 tajiri kwa viwanda na yale yanayoinukia-G20,yanayotaka pawepo hali ya uwazi kabisa katika kuteuliwa wakuu wa benki kuu ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF bila ya kuwepo masharti ni raia wa nchi gani.