1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwigizaji Baldwin amuua mwanamke wakati wa uigizaji

22 Oktoba 2021

Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya muigizaji wa Marekani Alec Baldwin kumfyatulia risasi kutoka bunduki inayotumiwa katika uchezaji filamu. Tukio hilo limefanyika wakati uigizaji wa filamu ulipokuwa unaendelea.

Alec Baldwin Schauspieler Set Film Dreh
Picha: Rich Polk/Getty Images for IMDb

Maafisa wanasema mwongozaji wa filamu Halyna Hutchins amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata na mwenzake Joel Souza amejeruhiwa pia katika tukio hilo.

Joel Souza amefikishwa katika kituo cha matibabu cha Santa FePicha: Sam Wasson/Getty Images

Afisi ya polisi ya mji wa Santa Fe inasema tukio hilo limefanyika wakati wa uigizaji wa filamu inayoitwa "Rust."

Maafisa wanasema Baldwin mwenye umri wa miaka 68 na ambaye ameonekana nje ya makao makuu ya polisi akilia, bado hajafunguliwa mashtaka yoyote.

Uigizaji wa filamu hiyo umesitishwa.

Halyna Hutchins ameuwawa kwa kupigwa risasiPicha: Fred Hayes/Getty Images for SAGindie

Hii si mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea, kwani Brandon Lee, ambaye ni mwanawe aliyekuwa gwiji wa filamu za Kung Fu Bruce Lee, alifariki dunia baada ya kupigwa risasi wakati wa uigizaji wa filamu ya "The Crow."

Mwaka 1984, mwigizaji Jon-Erik Hexum alifariki baada ya kujipiga risasi ya kichwa wakati wa uigizaji wa filamu ya "Cover Up."