Mwili wa Odinga kuagwa kitaifa mjini Nairobi
17 Oktoba 2025
Matangazo
Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa ibada hiyo itafanyika kwenye uwanja wa michezo wa Nyayo na kuongozwa na Rais William Ruto wa nchi hiyo.
Odinga, mwanasiasa kigogo wa upinzani aliaga dunia siku ya Jumatano akiwa nchini India alikokwenda kwa matibabu.
Mwili wake ulirejeshwa nyumbani jana Alhamisi na maelfu ya watu walipata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye uwanja wa Kasarani nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.
Hata hivyo zoezi hilo lilikumbwa na vurumai iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua watatu ya baada ya polisi kufyetua risasiili kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wakisongamana kuelekea jukwaa la watu mashuhuri.