Mwili wa Wangari Maathai kuchomwa moto.
4 Oktoba 2011Matangazo
Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel alifariki akiwa na umri wa miaka 71 baada ya kuugua saratani. Kwa mujibu wa uongozi wa Taasisi yake ya Greenbelt, misa maalum ya binafsi itafanyika siku ya Jumamosi na miti 5,000 itapandwa kote nchini Kenya kwa heshima yake. Je raia wa Kenya wanahisia gani kuhusu maombi ya marehemu Profesa Maathai? Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu wa Nairobi, Alfred Kiti.