1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwisho unaweza kuwa karibu

4 Februari 2016

Baada ya kutangaza hasara kubwa na kupunguza nafasi za ajira, mustakabali wa kampuni kubwa ya teknolojia ya Yahoo uko mashakani. DW inaangazia matatizo ya kampuni hiyo na juhudi za kuokoa biashara yake.

Marissa Mayer
Picha: picture alliance/AP Photo/J. Jacobson

Katika robo ya mwisho ya mwaka 2015, Yahoo ilipata hasara ya dola blioni 4.43 baada ya upunguzaji mkubwa wa thamani yake uliyotokana na ununuzi wa kampuni nyingine huko nyuma. Katika juhudi za kubadilisha hali, kampuni hiyo yenye makao yake jimboni California, ilitangaza kupunguza nafasi 1,500 za ajira, na kufunga ofisi katika miji mikubwa mitano duniani.

Lakini mchambuzi Martin Pyykkonen kutoka kampuni ya hisa ya Rosenblatt ya mjini New York, anasema hatua ya yahoo kupunguza wafanyakazi kama njia ya kurejesha ufanisi wa kampuni haingii akilini, na kwamba hapo kuna jambo linakosekana.

Lakini Mtendaji Mkuu wa Yahoo Marissa Mayer, anasisitiza kuwa anao mkakati wa ukuaji, ambao katika maneno yake, "utaboresha pakubwa mustakabali wao na kuongeza ushindani na kuwavutia watumiaji, watangazaji pamoja na washirika wao.

Mayer alisema Yahoo inapaswa kujikita katika shughuli kuu tatu za msingi kwa biashara ya wateja wao: Utafutaji, baruapepe na Tumblr, ambao ni mtandao wa blogi ya jamii iliyoupata mwaka 2013 kwa gharama ya dola bilioni 1.1.

Yahoo for sale

01:15

This browser does not support the video element.

Wawekezaji wanataka mabadiliko

Tumblr ni mmoja ya biashara kadhaa alizozichukuwa Myaer baada ya kuchukuwa usukani mwa Yahoo mwaka 2012. Lakini juhudi za kampuni hiyo kuingiza fedha zaidi kw akuwavutia watumiaji vijana zimeshindwa kuzaa matunda.

Tumblr ilishindwa kufikia lengo lake la kuingiza dola milioni 100 mwaka uliyopita, na Yahoo ikapunguza thamani ya kampuni hiyo kwa dola milioni 230. Kuyumba kwa biasgara ya yahoo katika miaka ya karibuni kumeathiri pia ufanisi wake katika masoko ya hisa, ambapo thamani yake ilishuka kwa zaidi ya asilimia 30 mwaka ulyopita, na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wawekezaji.

SpringOwl, kampuni ya usimamizi wa mali na mwanahisa katika yahoo, ilimkosoa Mayer kuwa ugawanyaji mbaya wa tajiriba, ushirika mbaya wa kimkakati, matumizi yasiyodhibitiwa na idadi kubwa ya wafanyakazi.

Brian Wieser, mchambuzi kutoka shirika la Pivotal Research, anaamini Yahoo inahitaji uongozi mpya. "Sijui kingine, alisema mchambuzi huyo na kusisitiza katika mahojiano na tovuti ya biashara ya Business Insider, kuwa ikiwa wanatka kujenga tena uaminifu, laazima aanguke.

Tayari kuuza

Kwa wakati huu bodi ya uongozi wa Yahoo imekataa miito kwa Mayer kujiuzulu na ilisema imejifunga kwa juhudi za timu ya uongozi kuibadili kampuni hiyo. Lakini mwenyekiti wa bodi ya yahoo Maynard Webb alisema kuwa ni katika maslahi ya wanahisa kujaribu mikakati mbadala.

Mara baada ya kauli yake hiyo, bei ya hisa za yahoo ilipanda kwa asilimia 5. Wawekezaji wanaitafsiri kauli hiyo kama kidokezo cha kutafuta mnunuzi. Lakini atakuw atayari kuinunua kampuni inayoyumba, na kwa bei gani?

Kufikia sasa, thamani ya hisa za yahoo ni dola bilioni 27. Lakini hiyo inatokana kwa sehemu kubwa na hisa zake katika tovuti ya bishara ya mtandao ya China, Alibaba. katika ripoti ya fedha ya karibuni ya yahoo, uwekezaji tu umewekwa kwa thamani kubwa ya dola bilioni 31, na hivyo kuchangia sehemu kubwa zaidi ya thamani jumla ya yahoo ambayo ni dola bilioni 45.

Hisa za Yahoo katika kampuni ya Alibaba zina thamani kubwa kuliko biashara yake kuu.Picha: picture-alliance/dpa

Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1994, awali ilikuwa ikijulikana kama Jerry's Guide to the World Wide Web. Kampuni hiyo ilipata mafanikio makubwa kama tovuti ya mtandaoni, lakini ilitokea kuwa na ufanisi mdogo ikilinganishwa na washindani wake wachanga kama vile Google na Facebook, katika kutumia idadi kubwa ya watumiaji kuongeza mapato ya matangazo.

Jerry Yang kujutia uamuzi wake

Miaka tisa iliyopita, mwanzono mwa mwaka 2008, hisa za yahoo zilikuw ana thamani ya chini kidogo tu ya dola bilioni 30, sawa na thamani yake ya sasa. Lakini wakati huo, kulikuwepo bado na matumaini ya mustakabali mwema, angalau katika mawazo ya Steve Ballmer, wakati huo mtendaji mkuu wa Microsoft.

Ballmer alitaka kuinunua yahoo kwa kiasi cha dola bilioni 44. Jerry Yang, mwanzilishi mwenza wa Yahoo na Mtendaji Mkuu wakati huo, alikataa pendekezo hilo, akiamini kampuni yake ilishushwa thamani. Ni uamuzi ambao anaweza kuja kuujutia.

Mwandishi: Becker Andreas
Mfasiri: Iddi Ssessanga
Mhariri: Saumu Yusuf

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW