Mwito wa Mfumo mpya wa katiba Visiwani Komoro
25 Aprili 2008Matangazo
Raia wengi, na hata wadadisi wa mambo ya kisiasa,wamekuwa wakizungumzia juu ya mfumo ulioko hivi sasa wa katiba ya visiwa hivi. Mfumo huu wa katiba, ambao kila kisiwa kina rais wake, ukiondoa yule wa Umoja wa Komoro, umekuwa ukipingwa sana na raia wengi Visiwani humu kwa kusema kwamba ndio unaodidimiza maendeleo ya visiwa hivyo.
Zaidi ni kutoka kwa Abdulrahman Baramia alioko Moroni.