1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 6,000

4 Januari 2026

Serikali ya kijeshi ya Myanmar imetoa msamaha kwa zaidi ya wafungwa 6,100 na kupunguza vifungo vya wafungwa wengine leo Jumapili wakati ikiadhimisha miaka 78 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka Uingereza.

Myanmar Yangon 2026 | Familia zinawakaribisha wafungwa walioachiliwa huru baada ya msamaha
Familia zinawakaribisha wafungwa walioachiliwa huru baada ya msamahaPicha: Thein Zaw/AP Photo/dpa/picture alliance

Serikali ya kijeshi ya Myanmar imetoa msamaha kwa zaidi ya wafungwa 6,100 na kupunguza vifungo vya wafungwa wengine leo Jumapili wakati ikiadhimisha miaka 78 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka Uingereza. Haijabainika mara moja kama walioachiliwa ni pamoja na maelfu ya wafungwa wa kisiasa waliokamatwa kwa kupinga utawala wa kijeshi.

Msamaha huo unatolewa wakati serikali ya kijeshi ikiendelea na mchakato wa uchaguzi wa hatua tatu kwa muda wa mwezi mmoja, ambao wakosoaji wanasema umeundwa ili kuipa sura ya uhalali hali iliyoko sasa.

Wafungwa wengine 52 ambao ni raia wa kigeni pia wataachiliwa na kufukuzwa nchini Myanmar. Hakuna orodha kamili ya walioachiliwa ambayo imetolewa. Wafungwa wengine walipunguziwa vifungo, isipokuwa wale waliopatikana na hatia ya makosa makubwa kama mauaji na ubakaji au waliokamatwa kwa makosa chini ya sheria mbalimbali za usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW