Myanmar yawezesha kiongozi wa mapinduzi kuwa rais wa kiraia
30 Machi 2026
Matangazo
Myanmar imesafisha njia kwa kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Jenerali Min Aung Hlaing kuwa rais wa kiraia nchini humo.
Hatua hiyo itamruhusu kuendeleza utawala wake wa mkono wa chuma lakini kama kiongozi wa kiraia.
Min Aung Hlaing ameitawala Myanmar tangu mwaka 2021 alipoongoza mapinduzi yaliyomng'oa Aung Suu Kyimadarakani na kukivunja chama cha Suu Kyi ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.
Mapinduzi hayo pia yalichochea vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Makamu watatu wa rais watachaguliwa, akiwemo mmoja wao atakayechaguliwa kuwa rais kwa kura ya bunge lote.