1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Israel waripuka katika mkutano wa kilele wa AU

5 Februari 2022

Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh ameuhimiza Umoja wa Afrika kukifuta kibali cha Israel cha kuwa mjumbe mwenye hadhi ya muangalizi, hatua inayoweka mazingira ya kuzuka mzozo wa ndani

Äthiopien | AU Gipfel in Addis Abeba
Picha: Shadi Hatem/APA Images/ZUMAPRESS/picture alliance

Hata wakati bara Afrika likikumbwa na msururu wa mapinduzi ya kijeshi na janga la corona, uhusiano na Israel unatarajiwa kuugubika mkutano huo.

Mzozo huo ulianza Julai mwaka jana wakati Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, kukubali kibali cha Israel kuwa na hadhi ya uangalizi kwenye umoja huo, hatua iliyozusha mzozo wa nadra ndani ya jumuiya hiyo ambayo inathamini maelewano.

Wakati wakuu wan chi walikusanyika katika mji mkuu wa Ethiopia Jumamosi, Shtayyeh aliuhimiza umoja huo kupinga hatua ya Faki.

"Israel haipaswi kutuzwa kwa ukiukaji wake na kwa utawala wa kibaguzi inaouwekea watu wa Kipalestina,” amesema.

Mkutano huo huenda ukashuhudia kura ikipigwa ya kuamua kama unaunga mkono au kupinga uamuzi wa Faki, ambao unaweza kusababisha mpasuko usio wa kawaida ndani ya jumuiya hiyo.

Palestina inapinga kibali cha Israel katika AUPicha: AFP/F. Arouri

Mapema Jumamosi, Faki alisema dhamira ya AU kwa harakati za uhuru wa Wapalestina "haijabadilika na inaweza tu kuendelea kuwa imara hata Zaidi”.

Amekitetea kibali cha Israel, hata hivyo, akisema kinaweza kuwa "chombo katika huduma ya amani” wakati akitoa wito wa kuwepo na "mdahalo wa tulivu” kuhusu suala hilo.

Wimbi la mapinduzi Afrika

Mataifa manne wanachama yamesitishwa kwa muda uwanachama na Baraza la Amani na Usalama la AU tangu katikati ya 2021 kwa sababu ya mabadiliko ya serikali yasiyo ya kikatiba – ya hivi karibuni ikiwa ni Burkina Faso, ambako wanajeshi walimuondoa Rais Roch Marc Christian Kabore mwezi uliopita.

Hii leo, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, anayehudhuria mkutano huo kwa njia ya video, anatarajiwa kutoa taarifa ya namna Afrika inavyolishughulikia janga la virusi vya corona, ikiwa ni karibu ya miaka miwili baada ya kisa cha kwanza kugunduliwa barani humo nchini Misri.

Umoja wa Afrika pia unakabiliwa na shinikizo la kuhimiza usitishwaji mapigano nchini Ethiopia., ambako vita vya miezi 15 vimewauwa maelfu ya wat una UN inasema, vimewaweka mamia kwa maelfu ya watu katika hatari ya baa la njaa.

Haijafahamika kama na vipi viongozi watauangazia mzozo huo, ambao unaihusisha serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na vikosi kutoka mkoa wa kaskazini wa Tigray.

afp

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW