Mzozo wa Ivory Coast
5 Desemba 2010Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amewasili nchini Ivory Coast kujaribu kuleta upatanishi katika mzozo wa uchaguzi ambao ulitarajiwa kumaliza mzozo uliodumu nchini humo kwa muongo mmoja, lakini badala yake umeufanya mzozo huo kuwa mgumu zaidi. Hii ni baada ya wagombea urais wote kuapishwa. Rais wa sasa Laurent Gbagbo aliapishwa, licha ya tume ya uchaguzi kumtangaza Alassane Ouattara kama mshindi. Hata hivyo baada ya muda wa saa kadha, Ouattara ambaye ni mgombea wa upinzani naye pia alidai kuwa rais. Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa kwa pamoja zimesema kuwa mshindi wa uchaguzi wa Jumapili iliyopita ni Ouattara. Ouattara alitangazwa mshindi na tume ya uchaguzi lakini hatua hiyo ilibatilishwa na baraza la katiba la nchi hiyo, taasisi ambayo inaongozwa na mshirika wa rais Gbagbo. Uchaguzi huo ulikuwa na lengo la kupoza majeraha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002, lakini badala yake unatishia kuanzisha upya hali ya wasi wasi